24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

Man City hatarini kufungiwa kusajili

MANCHESTER, ENGLAND

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Manchester City, wapo hatarini kufungiwa kusajili wachezaji kwa misimu miwili ijayo kutokana na kuvunja sheria za usajili zilizowekwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Inasemekana kwamba, timu hiyo tayari imefanyiwa uchunguzi na chama cha soka na Ligi Kuu England kutokana na usajili wa wachezaji wenye umri mdogo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za nje ya soka (financial fair play).

Hata hivyo, barua ya uchunguzi huo iliwasilishwa katika bodi ya uongozi wa mpira wa miguu barani Ulaya, UEFA, hivyo uchunguzi huo unaweza kuwafanya Manchester City wakafungiwa kusajili wachezaji kwa misimu miwili.

Hata hivyo, inasemekana kuwa Manchester City wanaweza kufungiwa hata kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa misimu miwili kama ilivyo kwa kutosajili.

Adhabu hiyo itakuja ikiwa ni mwezi mmoja baada ya Chelsea kukumbwa na adhabu kama hiyo kutoka kifungu cha 19 cha kanuni ya Fifa juu ya uhamisho wa wachezaji.

Hata hivyo, klabu hiyo ya Chelsea imekata rufaa juu ya adhabu hiyo na ndipo Fifa wakawaambia Chelsea bado adhabu hiyo haijafutwa, ila wanaendelea na uchunguzi ili kuweza kujiridhisha.

Fifa wamekuwa wakiwachunguza Manchester City kwa kipindi kirefu kwa uhamisho wa kimataifa, waliwahi kuchukuliwa hatua kutokana na uhamisho wa mchezaji, Benjamin Garre kutoka Velez Sarsfield mwaka 2016, ambapo uhamisho huo ulifanyika muda mfupi baada ya mchezaji huyo kusherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa na miaka 16.

Endapo Manchester City watakumbwa na rungu hilo, basi katika kipindi hicho cha misimu miwili hawatauza wachezaji wake kwa kuwa watashindwa kusajili wachezaji wengine kwa kipindi hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,231FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles