NA GLORY MLAY
SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa nchini (BFT) linatarajia kuandaa mashindano ya kimataifa yatakayofanyika Septemba 10, mwaka huu, Dar es Salaam.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, alisema mashindano hayo yatahusisha mabondia wa Tanzania na wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.
“ Mabondia wetu kwa sasa wapo kwenye mafunzo, wataanza mazoezi kwa ajili ya michuano hiyo ya kimataifa, ambapo Tanzania tutakuwa wenyeji,” alisema.
Alisema kuwa, lengo la mashindano hayo ni kutafuta mabondia watakaopambana na wenzao duniani na wengine kupata ajira katika timu za nje.
Mashaga alisema wadau na wapenzi wa ngumi wanatakiwa kujitokeza kwa ajili ya kusapoti mashindano hayo, kwani mpaka sasa hakuna wadhamini wa mchezo huo.