25.9 C
Dar es Salaam
Saturday, December 3, 2022

Contact us: [email protected]

MASHINDANO YA KIMATAIFA NGUMI SEPT 10

 

 

NA GLORY MLAY

SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa nchini (BFT) linatarajia kuandaa mashindano ya kimataifa yatakayofanyika Septemba 10, mwaka huu, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, alisema  mashindano hayo yatahusisha mabondia wa Tanzania na wengine kutoka nchi za Afrika  Mashariki na Kati.

“ Mabondia wetu kwa sasa wapo kwenye mafunzo,  wataanza mazoezi kwa ajili ya michuano hiyo ya kimataifa, ambapo Tanzania  tutakuwa wenyeji,” alisema.

Alisema kuwa, lengo la mashindano hayo ni kutafuta mabondia watakaopambana na wenzao duniani  na wengine kupata ajira katika timu za nje.

Mashaga alisema wadau na wapenzi wa ngumi wanatakiwa kujitokeza kwa ajili ya kusapoti mashindano hayo, kwani mpaka sasa hakuna wadhamini wa mchezo huo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,538FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles