NA JUMA HEZRON, TSJ
MSANII wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema anachukizwa na tabia ya mashabiki ambao wamekuwa wakifanya fujo kwenye shoo mbalimbali za wasanii.
Akizungumza na MTANZANIA leo, Ommy Dimpoz alisema kitendo hicho siyo cha kiungwana, mashabiki wamekuwa wakikosea na kuwavunjia heshima wasanii.
“Mashabiki wanatuogopesha, imekuwa kama jambo la kawaida kutufanyia vurugu na kusahau kuwa tunafanya shoo ili kuwapa burudani,” alisema Ommy Dimpoz.
Alisema mashabiki na wasanii ni watu wanaotegemeana kuhakikisha muziki wa Tanzania unapiga hatua, lakini hali imebadilika na sasa vurugu zimekuwa zikitawala.