24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

MASHABIKI NIGERIA KUCHUKIA USHINDI WA DIAMOND ITUFUNZE KITU

NA CHRISTOPHER MSEKENA


MWISHONI mwa wiki zilifanyika tuzo kubwa za muziki barani Afrika zinazoandaliwa na kituo cha runinga cha Sound City (Soundcity MVP  Awards Festival), katika hoteli ya Ecko huko Lagos, Nigeria.

Hizi ni tuzo ambazo zimejidhatiti kuweka uwazi, usawa na kusapoti zaidi muziki wa Afrika kwa ujumla bila kubagua utaifa, ndiyo maana utaona katika vipindi vyao, Sound City wana Top 10 ya muziki wa Afrika Mashariki.

Miongoni mwa washindi wa tuzo hizo ni msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye alishinda katika kipengele cha ‘Best Male MVP’, tuzo iliyokuwa inawaniwa na Davido, Wizkid, Cassper Nyovest Runtown, 2 Face , Olamide na Sarkodie.

Baada ya mwigizaji mkongwe kutoka Nigeria, Richard Mofe Damijo kutangaza ushindi wa Diamond Platnumz, mashabiki wa Bongo Fleva walizipokea kwa furaha taarifa hizo huku mashabiki wa muziki nchini humo waliokuwa kwenye ukumbi ule walionyesha kuchukizwa na kitendo hicho.

Baadhi ya mashabikio walisikika wakishangilia ‘OBO OBO OBO’ ambayo ni a.k.a ya Davido, wakimaanisha kutoridhishwa na ushindi wa Diamond Platnumz na yake walitaka msanii wao ndiyo ashinde tuzo hiyo.

Tovuti pendwa ya burudani nchini Nigeria, TheNet.ng imeripoti taarifa hiyo huku mashabiki wengine wa Nigeria wakionyesha chuki za wazi kwa kusema hawamjui, Diamond Platnumz zaidi ya kuijua benki ya Diamond Trust.

Kama shabiki wa kawaidi wa muziki kuna baadhi ya vitu ambavyo nimevibaini hapa ambavyo ni,

WANAPENDA VYAO

Kwanza nimegundua wale jamaa wanawapenda wasanii wao sana na hawapo tayari kuona msanii mwingine kutoka nje ya  Nigeria akichukua tuzo mikononi mwao.

Kama una kumbukumbu nzuri mwaka jana Alikiba alikumbana na matusi kutoka kwa mashabiki wa Wizkid baada ya kurudishiwa ile tuzo ya MTV Europe ambao awali aliishinda Star Boy.

Davido pia aliwahi kuwakejeli Diamond na Idris Sultan baada ya Chibu kushinda tuzo tatu za Chaneli O na Sultan kushinda, Big Brother Africa.

TUMEWAPA NAFASI NIGERIA

Katika muziki, Nigeria wanajipendelea zaidi kwa kucheza nyimbo za wasanii wao kuliko nyimbo za wasanii wengine na wanaamini hakuna msanii mwingine kutoka nje mwenye uwezo.

Sisi wenyewe tumekubali kuwapa nafasi kwa kucheza nyimbo zao wakati wao hawachezi ngoma zetu  kwa ukubwa tunaowapa. Ukiingia kwenye majumba ya starehe, utakutana na nyimbo za kina Davido, Wizkid na nyota wengine wa Nigeria.

Nyimbo za wasanii wetu hatuzipi nafasi ile inayostahili jambo ambalo linafanya mashabiki, Nigeria waamini wao ndiyo bora zaidi.

TUREKEBISHE HAPA

Kwanza kusiwakweze kwa kiasi kikubwa, binafsi naamini Bongo na Afrika Mashariki tuna wasanii wengi wakubwa wenye uwezo na endapo tukiwapa nafasi ambayo tunawapa wasanii wa Nigeria tutaweza kushindana nao vyema.

Lakini pia tunaweza kutengeneza umoja kama Afrika Mashariki, umoja utakaokuwa na nguvu ya kushindana kimuziki na Nigeria ambao hatuwezi kuwafikia bila kuwa kitu kimoja.

WASHINDI WENGINE

Mbali na Diamond Platnumz wasanii wengine walioshinda tuzo hizo ni Tiwa Savage (Best Female MVP), Cassper Nyovest (Best Hip hop), Sarkodie (Best Collaboration), Davido (Video Of The Year), Maleek Berry (Best Pop) na Wizkid (Dijital Artiste Of The Year).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles