25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

KASEKE: HALI NGUMU YA UCHUMI IMEONGEZA JITIHADA YA KUFANYA KAZI

Na ZAINAB IDDY


THAMANI ya miguu ya Deus Kaseke ilianza kuonekana alipokuwa katika kikosi cha Mbeya City chini ya kocha Juma Mwambusi kabla ya kusajiliwa na Yanga SC.

Lakini mwanzoni mwa msimu huu aliamua kujiunga na Singida United iliyopanda daraja na kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

SPOTIKIKI imezungumza na Kaseke ambaye ameweke wazi mitazamo yake katika masuala ya Kisiasa, Elimu, Uchumi na Jamii.

Elimu

“Kwa mjini suala la elimu linapewa kipaumbele na kufikia malengo ya serikali lakini, kwa upande wa vijijini bado   kwani zipo familia hazioni umuhimu wa kuwapeleka watoto wao shule jambo linalorudisha nyuma harakati za maendeleo ya nchini, hivyo ombi langu kwa seriali kupitia kwa wizara husika kuliangalia hili kwa jicho la tatu,”.

Uchumi

“Naipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuweza kufanya jitihada za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa wanachi wake Ingawa jamii inaonekana kuona hali ya uchumi ni ngumu lakini imesaidia sana kuongeza jitihada za kufanya kazi hata kwa watu ambao walikuwa hawaoni umuhimu kwa kutumia jasho lao kiharali kupata fedha za kuendesha maisha yao,”.

Jamii

“Dhama za kukatishana tamaa kudharauliana kwenye jamii bado zipo hili ni jambo linalokera na hata kuwafanya watu wengine wenye mioyo miepesi kushindwa kutimiza ndoto zao kwa kuhofia uenda watachekwa au kuonekana wamefanya mambo ya ajabu,”.

Siasa

“Yaani huko sipo kabisa kwa kuwa sina muda wa kufuatilia suala hilo  kwa kuwa mimi na siasa ni vitu viwili tofauti, ingawa napenda kuifuatilia kipindi cha kampeni kwaaji ya uchaguzi mkuu pekee tofauti na hapa wala sina muda nao wa kufuatilia na kutaka kujua,”.

Michezo

“Nje na soka napenda sana kusikiliza muziki pamoja na kucheza gemu au kutembelea marafiki na familia yangu,”.

Katika Ligi Kuu Tanzania Bara kikosi changu cha kwanza kitaundwa na Razak Abalola, Erasto Nyoni, Blues Kangwa, Kelvin Yonda, Kennedy Juma, Mudathir Yahaya, Shiza Kichuya, Papy Tshishimbi, Ibrahim Ajib Emmanuel Okwei na Habibu Kiyombo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles