27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MASHABIKI 100,000 WAKUTANA BRAZIL KUOMBOLEZA

CHAPECO, BRAZIL


ZAIDI ya mashabiki 100,000 wa klabu ya Chapecoense na klabu ya Atletico Nacional, usiku wa juzi kuamkia jana walikutana nchini Brazil kwa ajili ya kuomboleza vifo vya wachezaji wa klabu ya Chapecoense.

Klabu hiyo ya Chapecoense imepoteza wachezaji wake mwanzoni mwa wiki hii kutokana na ajali ya ndege iliyotokea katika anga ya nchini Colombia ambapo abiria 71 walipoteza maisha pamoja na wachezaji wa timu hiyo.

Timu hiyo ilikuwa inakwenda nchini Colombia kwa ajili ya kucheza na Atletico Nacional kwenye mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Copa Sudamericana. Kutokana na tukio hilo, mashabiki wa klabu hiyo ya nchini Colombia waliamua kusafiri hadi nchini Brazil ili kujiunga na wenzao kuomboleza vifo hivyo.

Mashabiki wengine zaidi ya 45,000 waliobaki nchini Colombia, walikutana kwenye uwanja wa Atanasio Giradot ambao ulitakiwa kupigwa mchezo huo, huku wakiwa wamevaa T-shirt nyeupe na wakiwa wamewasha mishumaa na kuchukua maua.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Brazil nchini Colombia, Jose Serra, alijiunga na mashabiki hao kwa ajili ya kufanya maombolezo.

“Kutoka moyoni mwangu, nawashukuru mashabiki wa hapa nchini Colombia kwa kukutana pamoja kwa ajili ya kuomboleza vifo vya wachezaji wetu, Colombia wameonyesha jinsi gani walivyoguswa na tukio hilo, umoja wenu unatufanya tujisikie furaha,” alisema Serra.

Kwa upande wa mashabiki wa Chapecoense waliojitokeza kwenye uwanja wao kwa ajili ya maombolezo, walikesha huku wakiwa wanaimba nyimbo mbalimbali na kucheza, huku wachezaji wachache ambao hawakusafiri na ndege hiyo na kubaki kwenye klabu yao, waliungana na baadhi ya viongozi na kuzunguka kwenye uwanja huo wakiwapungia mikono mashabiki wao.

Kwa upande England, kulikuwa na baadhi ya michezo ambayo iliendelea katika michuano ya Kombe la Ligi hatua ya robo fainali, katika kila mchezo kulikuwa na dakika ya utulivu kwa ajili ya kuomboleza.

Klabu kubwa nchini Brazil zimedai kuwa zipo tayari kutoa wachezaji wao kwa mkopo na kujiunga na Chapecoense kwa ajili ya misimu mitatu ya ligi ili kuilinda klabu hiyo isishuke daraja.

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ametuma salamu za pole kwa chama cha soka nchini Brazil pamoja na nyota wa zamani wa soka nchini humo Pele na nyota wa sasa wa timu hiyo ya taifa na klabu ya Barcelona, Neymar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles