26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yaonywa uwezekano wa kusambaa zaidi Covid-19

WASHINGTON, MAREKANI

DAKTARI wa ngazi ya juu wa Magonjwa ya maambukizi nchini Marekani amewaonya maseneta kuwa virusi vitasambaa iwapo nchi itafungua shughuli zake mapema sana.

Dk. Anthony Fauci alisema jana kuwa miongozo ya shirikisho ya kufungua shughuli za kibiashara tena haitafuatwa, “maambukizi madogo madogo” yatakua mlipuko.

Alisema pia kwamba idadi halisi ya vifo nchini Marekani huenda ikawa kubwa kuliko idadi rasmi inayotolewa ya vifo 80,000.

Ujumbe wake uko kinyume na taarifa iliyotolewa na Rais Donald Trump ambaye yuko makini kutaka shughuli za kiuchumi zifunguliwe tena.

Dk. Fauci alikua akizungumza kwa njia ya video na kamati ya seneti inayoongozwa na Republican nchini Marekani.

Alikua akielezea kuhusu mpango wa kufunguliwa upya kwa shughuli Marekani baada ya majimbo zaidi ya 12 kuweka amri ya kukaa nyumbani ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona ambao unajumuisha awamu ya siku 14 ambazo majimbo yanaombwa kuzifuata wakati wanaporuhusu kufunguliwa kwa shule na biashara.

Majimbo kadhaa ya Marekani ambayo tayari yamekwishaanza tena shughuli zao za kiuchumi yana viwango vya juu vya ongezeko la maambukizi, badala ya kushuka.

Olionya kuhusu kusababisha mlipuko ambao maofisa hawataweza kuudhibiti, akiongeza kuwa mlipuko wa aina hiyo utarudisha nyuma kufufuka kwa uchumi na unaweza kusababisha “kuugua na vifo”.

Ingawa Ikulu ya White House imeweka miongozo ya kufungua shughuli za kiuchumi, ni jukumu la magavana kuamua juu ya namna ya kulegeza sharia za kukaa nyumbani zilizowekwa.

“Bila shaka, hata katika hali nzuri sana, ukipunguza hatua za kudhibiti maambukizi utaona visa vinajitokeza,” Dk. Fauchi aliwaonya maofisa wa Marekani.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kurejea tena wa virusi wakati wa majira ya vuli, Dk. Fauci alisema “inawezekana au isiwezekane”.

“Ninatumai kwamba kama tuna tisho la wimbi la pili tutaweza kukabiliana nalo kwa ufanisi zaidi kama utakuwa mlipuko,” alisema. 

Dk. Fauci pia alisema kuwa kuna chanjo nyingi ambazo zinatengenezwa lakini anatumai zitaweza kufikia viwango hitajika.

Mashahidi walionekana kwa njia video kwakati wa kikao cha zaidi ya saa tatu, sawa na walivyofanya maseneta wa Kamati ya Masuala ya Afya, Elimu na Malipo ya uzeeni.

Wajumbe watatu wa kikosi kazi cha kupambana na virusi vya corona cha Ikulu ya White House walitoa ushahidi wao wakiwa karantini baada ya kuwa na uwezekano wa kuugua akiwemo Dk. Fauchi.

Mkurugenzi wa Vituo vya Kuudhibiti na Kuzuwia ugonjwa Dk. Robert Redfield na kamishna wa taasisi ya Marekani ya Utoaji wa taarifa, Stephen Hahn pia wamejitenga binafsi kutokana na uwezekano wa kupata maambukizi ya virusi.

Dk. Fauci hakupatikana na virusi alipopimwa lakini ataendelea kufanyia kazi nyumbani kwa sasa, na atakuwa akipimwa mara kwa mara.

Kikao kiliongozwa na seneta wa Republican kutoka jimbo la Tennessee Lamar Alexander akiwa nyumbani kwake eneo la Smoky Mountains. Mbwa wake aina ya Rufus alikua akionekana mara kadhaa akizunguka nyuma yake wakati wa kikao cha njia ya video.

“Kukaa nyumbani daima sio suluhu la janga hili. Hakuna pesa za kutosha zilizopo za kuwasaidia wale wote wanaoumizwa na kufungwa kwa shughuli za kiuchumi,” alisema 

alisema Alexander.

Seneta wa Washington Patty Murray, mwenye cheo cha juu katika kamati ya Democratic, alikasirika kwamba  Trump anataka zaidi “kupambana zaidi na ukweli kuliko kupambana na virusi “.

Serikali haiwezi kuwaomba watu kuanza upya maisha yao ya kawaida “kama hakuna maelezo ya wazi ya muongozo juu ya jinsi ya kufanya hilo kwa usalama “, aliongeza.

Wakati huo huo Makamu Rais, Mike Pence pia yuko mbali na Rais Trump baada ya ofisa wake wa habari, Katie Miller kupatikana na virusi vya corona baada ya kupimwa wiki iliyopita.

“Makamu wa rais amefanya chaguo lake la kukaa mbali kwa siku chache,” alisema ofisa wa habari wa White House Kayleigh McEnany.

Ushahdi wa Dk. Fauci mbele ya kamati ulianza kama mazungumzo ya kawaida ya busara, huku maseneta wakimchukulia kama afisa wa huduma za afya wa muda mrefu ambaye ushauri wake unaonekana una mamlaka na wenye utaalamu.

Ni ushahidi wa kuongezeka kwa mgawanyiko wa kisiasa ndani yataifa juu ya jinsi ya kukabiliana na virusi na ni lini, wanapaswa kuanza kulegeza amri zilizopo kwa sasa za juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles