24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Darasa: Ninafanya wanachotaka mashabiki

Na GLORY MLAY

MSANII wa miondoko ya Hip hop nchini, Sharif Ramadhan ‘Darasa’, amesema siri iliyopelekea nyimbo zake kukubalika ni kutambua wanachotaka mashabiki wa muziki wake.

Darasa aliliambia MTANZANIA kwamba katika ushindani wa sasa, msanii hatakiwi kukurupuka, bali anatakiwa atambue mashabiki wake wanataka nini na kwa wakati gani.

“Mwanzo nilikuwa nikitoa nyimbo zenye vionjo vyenye ujumbe wa kutosha lakini hazikuwa zikipokelewa sana ila nilipokaa na kufikiria zaidi, nikatambua nini mashabiki wanataka na ndiyo maana muziki wangu upo juu sana tofauti na zamani,” alisema.

Alisema kitu kingine ambacho kinapelekea muziki kuwa mzuri ni utunzi, mashairi pamoja na kutambua prodyuza anayeendana na unavyotaka muziki wako uwe.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles