24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Rajoelina awaponda wanaodhalilisha wanasayansi wa Kiafrika

ANTANANARIVO, MADAGASCAR

RAIS Andry Rajoelina wa Madagascar amezikosoa vikali nchi za Ulaya kwa kutilia shaka dawa ya asili inayodaiwa kutibu ugonjwa wa Covid-19 iliyozinduliwa na nchi yake akisisitiza kuwa, iwapo dawa hiyo ingelikuwa imegunduliwa katika nchi za Ulaya, isingetiliwa shaka.

Rais Rajaoleina amesema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya France 24 ya Ufaransa na kueleza bayana kuwa, “wanasayansi wa Kiafrika hawapaswi kudhalilishwa na kuonwa duni.”

Rais huyo wa Madagascar alihoji, “iwapo ni nchi ya Ulaya ingeligundua dawa hii, kungekuwa na shaka kiasi hiki? Sidhani!”

Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na kutahadharisha juu ya matumizi ya dawa hiyo inayofahamika kama Covid Organics, liliwataka viongozi wa Serikali ya Antananarivo kuifanyia utafiti wa kitiba.

Aidha Umoja wa Afrika (AU) umeitaka Madagascar kuweka wazi matokeo ya uchunguzi wa kitaalamu kuhusiana na taathira na usalama wa dawa hiyo.

Hata hivyo, nchi za Afrika zikiwemo Niger, Equatorial Guinea, Senegal, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania tayari zimekwishaagiza dawa hiyo kwa ajili ya kuifanyia utafiti. 

Licha ya Madagascar kusajili kesi 193 za waathirika wa virusi vya Corona, lakini hakuna mtu yeyote nchini humo aliyethibitishwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Rajoelina alisema kwamba Taifa la Ulaya lingekuwa limetenegenza dawa hiyo, majibu ya mataifa ya magharibu yabgekuwa tofauti

Rajoelina amesema kwamba wakosoaji wa dawa ya mitishamba ambayo haijajaribiwa ambayo anaipigia debe kuwa tiba ya Covid-19 inaonyesha tabia ya ubwenyenye ya mataifa ya magharbi dhidi ya Afrika.

Mkutano wa wataalam 70 wa dawa za kitamaduni Afrika umeafikiana na kwamba dawa zote zinapaswa kufanyiwa majaribio miongoni mwa binadamu, kulingana na shirika la Afya duniani tawi la Afrika ambalo lilichapisha katika twitter.

AFP

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles