24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yalaumiwa kuua wasio na hatia Somalia

MOGADISHU, SOMALIA

MAJESHI ya Marekani yanayoendesha mashambulizi ya anga nchini Somalia dhidi ya ngome za wapiganaji wa Al-Shabab yamelaumiwa kuwaua raia wasio na hatia.

Kwa mujibu wa Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International (AI), katika mashambulizi matano iliyochunguza watu 14 waliuawa na wengine saba kujeruhiwa.

Hata hivyo, Marekani imekana taarifa hizo. Lakini  kwa mujibu wa Ofisa wa AI, Seif Magango mashambulizi hayo yaliwalenga raia wasio na hatia waliokuwa wakiendelea na shughuli za kawaida na ambao hawakuwa na uhusiano wowote na kundi la al-Shabab.

Magango amesema kuwa mashambulizi hayo yalifanyika katika jimbo la Lower Shebelle katika mitaa kadhaa ikiwemo Faraweis, Darusalaam na Ilimei.

Katika Faraweis watu saba waliuawa ikiwemo wanawake na watoto huku wakulima watatu waliokuwa wakiendelea na shughuli zao za kilimo wakipigwa kombora na kuawa papo hapo katika eneo la Darusalaam.

Afisa huyo amesema kuwa hali hiyo ilianza tangu Rais Donald Trump alipotangaza kuwa jeshi lake litakuwa likitumia ndege zisizo na rubani kukabiliana na wapiganaji hao.

”Tangu Rais Trump aingie madarakani kumekuwa na mashambulizi zaidi ya 100 na tunachojiuliza ifikapo mwisho mwa mwaka huu wangapi watakuwa wameuawa,” alihoji.

Lakini saa chache tu baada ya kutoa ripoti hiyo, Jeshi la Marekani lilitoa taarifa yake likikanusha taarifa hizo na kusema kuwa kikosi chao cha AFRICOM huzuia mauaji ya raia wasio na hatia.

Katika taarifa hiyo AFRICOM inasema lengo la mashambulizi yake ni kuwalinda raia wa Somalia dhidi ya ugaidi mbali na kuisaidia Serikali ya Somalia kukabiliana na changamoto za kiusalama.

”AI ilitoa ripoti ikidai kwamba mashambulizi manane ya AFRICOM kati ya 2017 na 2018 yalisababisha vifo vya raia. Tunashukuru juhudi za AI kuturuhusu kuchangia katika ripoti hiyo kabla ya uchapishaji wake licha ya kwamba tunaamini kwamba si ya ukweli, ilisema taarifa hiyo”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles