Maalim Seif atinga Ofisi za ACT Zanzibar, arushiwa mchele kumuepusha na husda

0
3536

Mwandishi Wetu, Unguja

Kwa mara ya kwanza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, amewasili visiwani Zanzibar akiwa mwanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Maalim Seif aliwasili visiwani humo jana, ambapo leo Alhamisi Machi 21, amekwenda kwenye Ofisi za Chama cha ACT-Wazalendo, Vuga mjini Unguja, ofisi ambazo awali zilikuwa za CUF.

https://twitter.com/MtanzaniaNews/status/1108644456130056195

Maalim Seif amelakiwa na mamia ya wafuasi wa ACT-Wazalendo waliokusanyika katika ofisi hizo kwa namna ya pekee huku  wakimrushia mchele ambapo wenyeji wanasema tafsiri yake ni kumuepusha na husda na jicho baya.

Maalim Seif anatarajiwa kuzungumza na wanachama hao mjini Unguja ikiwa ni mara ya kwanza tangu ahame kutoka CUF.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here