Kampala, Uaganda
Balozi wa Marekani nchini Uganda, Natalie Brown ameeleza kusikitishwa na hatua ya serikali ya kukataa kuwapatia wasimamizi wao idhini ya kusimamia uchaguzi.
Balozi Brown amesema kuwa zaidi ya asilimia 75 ya maombi ya idhini za ujumbe wa wakaguzi wa Marekani yalikataliwa.
Ni watu 15 pekee ndio waliopewa idhini hiyo, lakini ubalozi huo unasema idadi hii haitoshi kufuatilia uchaguzi.
Brown ameongeza kuwa Tume ya Uchaguzi haikutoa maelezo yoyote juu ya ni kwanini maombi yao yalikataliwa, ingawa ubalozi huo uliwasilisha nyaraka zote zinazohitajika.
Kupitia ujumbe wa Twitter Balozi Brown alisema kuwa anasikitika kutangaza uamuzi wa Marekani wa kutosimamia uchaguzi wa Uganda baada ya asilimia 75 ya maombi ya idhini ya kusimamia uchaguzi kukataliwa: