30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani waichapa Thailand mabao 13

REIMS, UFARANSA 

TIMU ya taifa ya soka ya Wanawake ya Marekani, imeanza kuonesha dalili ya kutetea taji la Kombe la Dunia baada ya juzi kuwachapa wapinzani wao Thailand mabao 13-0.

Marekani wanataka kuendelea kuweka historia kwenye michuano hiyo ikiwa wanashika nafasi ya kwanza kwa kutwaa taji hilo mara nyingi kuliko taifa lolote, wamechukua jumla mara tatu.

Michuano hiyo inaendelea huko nchini Ufaransa, huku timu 24 kutoka Mataifa mbalimbali zikioneshana nguvu, lakini juzi Marekani walionekana kuwa wanataka kutetea taji hilo kutokana na kiwango walichokionesha.

Katika ushindi huo, mshambuliaji wa Marekani ambaye pia ni nahodha Alex Morgan, alikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu huku akipachika mabao matano peke yake, wakati huo Rose Lavele akipachika mabao mawili na mabao mengine yakifungwa na Lindsey Horan, Sam Mewis, Megan Rapinoe, Mallory Pugh na Carli Lloyd.

Alex amedai wamekwenda kwenye mashindano hayo kwa ajili ya lengo la kutetea ubingwa na kuandika historia mpya.

“Tumekuja kufanya kweli kwenye michuano hii mikubwa duniani, kila bao linaonesha jinsi gani tulivyo jiandaa, tunajua ushindani utakuwa mkubwa, lakini tuna kila sababu za kutetea ubingwa,” alisema nahodha huyo.

Michezo mingine ambayo ilipigwa juzi ni pamoja na Uholanzi ambayo ilishinda bao 1-0 dhidi ya New Zealand na Chile wakipigwa 2-0 dhidi ya Sweden.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles