28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Marafiki wa Lowassa kuchangia damu Muhimbili

LOWASSAAANA ELIYA MBONEA, ARUSHA
MAKAMU Mwenyekiti wa marafiki wa Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Angel George, amesema mipango imekamilika ya kwenda kuchangia damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
George alitoa taarifa hiyo jana jijini hapa, baada ya kusoma taarifa kwenye vyombo vya habari ikieleza kwamba, Hospitali ya Taifa Muhimbili inakabiliwa na uhaba wa damu.
“Hii taarifa tumeiona, tayari tumewasiliana na marafiki wa Lowassa waitwao Friends of Lowassa nchi nzima na naamini tukimaliza kikao leo, safari ya kwenda kuchangia damu kule Muhimbili ili kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu itakuwa tayari.
“Kwa hiyo naomba nitumie fursa hii kuwaomba Watanzania wenzetu wanaojali na kuthamini maisha ya Watanzania wote, wajitokeze ili kufanikisha uchangiaji wa damu,” alisema George.
“Sisi ambao ni marafiki wa Lowassa, tumeamua kufanya shughuli hizo za kuisaidia jamii ili kumuunga mkono na kumhamasisha Lowassa anayetarajiwa kutangaza nia hivi karibuni ya kuwania urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles