25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

John Nyerere azikwa Butiama

Na Fredrick Katulanda, Butiama
ASKOFU wa Kanisa Katoliki jimbo la Musoma, Michael Msonganzila, ameongoza ibada ya mazishi ya mtoto wa nne wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, John Nyerere.

John alifariki dunia Mei 9 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Mahimbili, alipokuwa akipatiwa matibabu na jana alizikwa kijijini kwao Mwitongo wilayani Butiama, ambako viongozi mbalimbali wa taifa walihudhuria.

Miongoni mwa waliohudhuria mazishi hayo ni viongozi wa vyama vya siasa, wabunge huku Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro, akiiwakilisha Serikali katika msiba huo.

Wengine ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Stephen Kebwe, na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Amina Makilagi.

Akizumgumza katika ibada ya hiyo mazishi, Askofu Msonganzila, alisema kifo cha John Nyerere kinakumbusha maisha ya duniani yapo safarini na kwamba hakuna njia ya kufika mbinguni bali kupitia kifo.

Alisema mwanadamu anahimizwa kusali na kuomba kwa vile akishakufa hana uwezo wa kujiombea hivyo anahitaji kuombewa na waliosalia duniani.

Hata hivyo wakati ibada hiyo ikiendelea Askofu Msonganzila, alilazimika kukatisha ibada kwa baada ya kuwasili Lowassa baada ya umati wa watu ulimiminika kutaka kusalimiana na waziri mkuu huyo wa zamani.

Kutokana na hali hiyo, iliwalazimu wasimamizi wa ibada kuwatuliza watu waliokuwa wakipita katika viti vya mbele na kwenda kusaliamiana na Lowassa kuruhusu misa ya ibada iendelee.

Baada ya watu kutulia ndipo Lowassa alipopata wasaa wa kwenda kwa Mama Maria Nyerere kumpa mkono wa pole na ibada kuendelea.

“Maisha yetu hapa duniani ni safari kutoka kuzaliwa hadi kufa, yeye John amemaliza safari yake na sasa hana uwezo wa kujiombea tunaopaswa kumuombea ni sisi tulio hai,” alisema.

Akitoa salamu za Serikali katika msiba huo, Waziri wa Katiba na Sheria,Asha-Rose Migiro, alisema Serikali inatambua kazi ya marehemu John wakati wa vita ya Uganda ambako alikuwa mstari wa mbele kuikomboa nchi.

Kwa vyama vya siasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliwakilishwa na Katibu wa Itikadi na Mwenezi, wake, Nape Nnauye, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyewakilisha alikuwa Meya wa Manispaa ya Musoma, Alex Kisulula na Chama cha ACT Wazalendo, kiliwakilishwa na Mwenyekiti wake, Anna Mghwira.

Kwa upande wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambako John Nyerere aliwahi kuwa rubani wa ndege vita, Brigedia General Mathew Sukambi alitoa salamu za rambirambi na kueleza kuwa kifo cha John kilipokelewa kwa masikitiko makubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles