30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mapya yaanza kuibuka mwandishi aliyetoweka

ISTANBUL, UTURUKI

VYOMBO vya habari nchini hapa vimechapisha picha za kamera za usalama – CCTV ambazo zinaonesha ushahidi wa njama iliyohusishwa na mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi kutoweka.

Picha za vyombo hivyo vya habari zinawaonesha maofisa usalama wa Saudi Arabia wakiingia na kuondoka nchini hapa kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa uliopo mjini hapa.

Khashoggi ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Saudi Arabia, mara ya mwisho Oktoba 2 mwaka huu alionekna akiingia katika ubalozi wa nchi hiyo uliopo mjini hapa na tangu siku hiyo hajawahi kuonekana tena.

Mamlaka za hapa zinadai Khashoggi aliuawa akiwa ndani ya ubalozi huo, lakini Saudi Arabia wanakanusha madai hayo.

Kituo cha televisheni cha TRT World channel Kwa kilichorusha picha hizo jana, kilidai kuzinasa kutoka kwenye kamera za usalama.

Picha hizo zinaonesha magari yakiwasili kwenye ubalozi huo likiwamo gari jeusi ambalo linasadikika kuwa ni la mkuu wa usalama.

Picha hizo zinalionesha pia kundi la wanaume wakiingia nchini kupitia uwanja huo wa ndege na wakianza kutafuta hoteli kabla ya kuondoka nchini.

Gazeti la Sabah la nchini hapa liliripoti kuwatambua wanausalama 15 ambao walihusika na kutoweka kwa mwandishi huyo.

Vyombo vya habari vya hapa vinadai pengine Khashoggi angetekwa na wala asingeuawa.
Mbali na taarifa hizo za vyombo vya habari, polisi walidai kuwa wanazichunguza kamera za usalama 150 kama sehemu ya upepelezi wao.

Wapelelezi hao walisema pia wanaifuatilia ndege ya Saudi Arabia aina ya Gulfstream iliyowasili Oktoba 2, mwaka huu ambayo picha hizo zinaionesha ikiwa imeegeshwa uwanjani hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles