26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mapigano Yemen yakatisha safari ya Rais Uhuru Kenyatta

Uhuru-Kenyatta1NAIROBI, Kenya,

NDEGE iliyokuwa imembeba Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, imelazimika kukatisha safari na kurejea nyumbani baada ya kuwapo hofu ya hali ya usalama katika eneo la anga ya Yemen.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo, Manoah Esipisu, tukio hilo lilitokea wakati Rais Kenyatta akiwa safarini kuelekea Dubai.

Esipisu alisema hali hiyo ilitokana na changamoto ya usalama baada ya kuwapo kwa mapigano yanayoendelea nchini Yemen baina ya jeshi la nchi hiyo na wanamgambo wa Houthi.

Gazeti la The Standard limemkariri Esipisu akisema kuwa Rais Kenyatta alikuwa anakwenda Dubai kwa ajili ya kuunganisha safari ya kuelekea Los Angeles, Marekani.

“Hali hiyo inatokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya kijeshi nchini Yemen, kumekuwapo na changamoto safari za anga kupitia eneo hilo, hivyo tukaamua kurudi nyumbani…Rais alitua katika Kiwanja cha Ndege cha Jomo Kenyatta saa tano usiku wa kuamkia leo (juzi),”alisema Esipisu.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles