Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital
Askofu wa Kanisa la Good News for all Ministry, Dk. Charles Gadi, ameongoza maombi maalum ya kuombea mvua kwa Taifa la Marekani ambalo limekubwa na ukame kwa muda sasa.
Akizungumza na waandishi was habari Dar es Salaam leo Desemba 21, 2022 amesema kuwa msukumo wa maombi haya ni baada ya kupata taarifa ya kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ikiwamo taarifa rasmi juu ya hali ya ukame uliolikumba taifa hilo kubwa duniani.
Aidha, amesema kuwa ukame ambao haujawahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa ambapo hali hii imesababisha ukame katika vyanzo mbalimbali vya maji yaliyo chini ya ardhi.
“Tunaamini pia huu ni wakati ambapo Mungu anafungua mlango ili taifa la Marakeni liweze kuhitaji msaada kutoka Tanzania, ambao ni huu wa maombi maalum ya kupata mvua nyingi na tunaamini kupitia hili Mungu atafungua uhusiano kati ya Tanzania na Marakeni,” amesema Gadi.
Aliongeza kuwa hii ni dhahili kuwa taifa hilo na mataifa mengine yanamhitaji Mungu ili aingilie Kati kwani pamoja na utalaamu wao wa kisayansi na fedha zao lakini bado hawana majibu ya hili la ukame ambapo kwa Mungu Hana mwisho .
Aidha, aliongeza kuwa enzi za uongozi wa baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere, Tanzania iikumbwa na uhaba wa chakula kiasi kwamba alikwenda Marekani kuomba msaada wa chakuka na taifa likaweza kupata unga wa njano ambo kwao ulikuwa ukitumika kulishia wanyama lakini hata hivyo ulifaa na kusaidia nchi kuondokana na janga la njaa.