26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Halopesa kuzindua ‘Shinda tena na Halopesa’

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel, inaendelea kuwahamasisha wateja wao kwa kuleta huduma za ubora zenye ubunifu kwa kuzindua Kampeni ya “SHINDA TENA NA HALOPESA’.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Halotel, Magesa Wandwi, amesema kuwa Halotel inafuraha kubwa kutoa huduma za kifedha na kuwawezesha wateja kufanya miamala toafuti tofauti .

Aidha, amesema mteja anaweza kutuma pesa Halotel kwenda Halotel na mitandao mingine, kutuma pesa kwenda benki, kulipia bili nakadhalika ambapo wateja zaidi ya million 2.5 ni wateja hai na wanaendelea kufuarahia huduma zenye ubora kwa gharama nafuu mda wowote.

“Kampeni ya SHINDA na HALOPESA ni kwa ajili ya kuwapa hamasa wateja wake ili waweze kuendelea kutumia huduma zetu za kidigitali ili waweze kuingia kwenye ulimwengu huu, huku ndoto yetu ikiwa ni kuona Watanzania wote wanatumia huduma za kifedha kiganjani mwao,” amesema Magesa.

Kwa upande wa Afisa Masoko was HALOPESA, Roxana Kadio, amesema Kampeni hiyo ni kwa ajili ya wateja wa Halopesa amabayo itakuwepo kwa miezi mitatu na wateja 135 wataweza kuwa washindi, wateja 120 watashinda pesa taslimu na wateja 12 wataweza kishinda Luninga janja na wengine watatu watashinda bajaji mpya.

“Kila mteja wetu anaalikwa kushiriki katika Promosheni hii kwa kufanya miamala Kama , kutuma hela Halopesa kwenda Halopesa, kutuma hela mitandao mingine, kutuma hela benki , malipo ya kiserikali , lipa bili, lipa hapa, kutoa pesa kupitia wakala kutoa pesa kutoka ATM pamoja na miamala ya Halo yako,” amesema Kadio.

Hata hivyo, Halopesa inafuraha kuzindua Promosheni hii leo na itanendelea kufikiria njia nyingne zaidi za kufanya ulimwengu wa huduma za kifedha kupitia simu kuwa bora zaidi kwa ajili ya wateja wetu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles