23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 11, 2024

Contact us: [email protected]

TEF: Kuna dalili njema mabadiliko ya sheria

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) limesema kuna dalili njema katika kupata mabadiliko ya sheria ya Vyombo vya Habari nchini na kwamba wanaimani kubwa na Serikali.

Hayo yameelezwa Juzi na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deodatus Balile wakati akizungumza na Mtanzania Digital ambapo alikiri kuwa kuna hatua nzuir ambayo imefikiwa baina yao na Serikali katika kikao cha mwisho.

“Ni kweli kabisa kwamba tumefikia hatua nzuri kwani katika kikao cha mwisho tulikubaliana kwamba mapendekezo hayo yapelekwe kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili yaandikwe kwenye msingi wa kisheria kisha yapelekwe bungeni.

“Ni imani yetu kwamba yale yote tuliyopendekeza yatakuwemo kwa ajili ya ustawi wa tasnia ya habari, hivyo tunaona dalili njema za kulifanikisha hili,” amesema Balile.

Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa ratiba, bunge lijalo litakuwa Januari 31, 2023 ambalo ndilo linatarwajiwa kupokea mapendekezo hayo.

Desemba 6, mwaka huu serikali kupitia kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ilisema kuwa inajiandaa kuwasilisha bungeni mabadiliko ya Sheria zinazohusu Vyombo vya Habari nchini ili wabunge wakiridhia utekelezaji wake ufanyike huku ikihimiza kuwa dhamira yake katika tasnia hiyo ni njema.

Msigwa alisema kuwa anatambua kuwa katika tasnia ya habari kuna changamoto na moja ya changamoto ni kuhusu sheria zinazohusu vyombo vya habari ambazo amesema kuwa zinahitaji kurekebishwa na kwamba wamekamilisha majadiliano ngazi ya wadau.

Mchakato wa mabadiliko ya sheria zinazominya uhuru wa habari nchini, ulishika kasi baada ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuagiza serikali na wadau kukaa pamoja na kuangalia namna ya kumaliza kero hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles