25.4 C
Dar es Salaam
Thursday, January 9, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Maofisa 26 JWTZ washindwa kuhitimu

Na NORA DAMIAN

MAOFISA 26 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wameshindwa kuhitimu mafunzo yao kutokana na sababu mbalimbali.

Maofisa hao ambao walianza masomo Januari 28, mwaka jana katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA), walipaswa kuhitimu jana na wenzao.

Akizungumza jana wakati wa kutunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa JWTZ kundi la 67/19, katika cheo cha Luteni Usu, Mkuu wa Chuo cha TMA, Brigedia Jenerali Ibrahim Mhona, alisema katika kozi hiyo kulikuwa na wanafunzi 126 na kati yao wanaume walikuwa 101 na wanawake 25. 

“Maofisa wanafunzi 26 waliachishwa mafunzo kwa sababu mbalimbali zikiwemo za ugonjwa, kushindwa kufikia viwango vya ufaulu na kukimbia mafunzo,” alisema Brigedia Jenerali Mhona.

Alisema pia maofisa wanafunzi 28 walijiunga baada ya kufanya mafunzo nje ya nchi na kati yao 10 walikuwa China, India (2), Kenya (5), Morocco (9), Uingereza mmoja na Ujerumani mmoja.

Katika hafla hiyo, Rais Dk. John Magufuli aliwatunuku kamisheni maofisa 128 na kati yao wanaume ni 108 na wanawake 20.

Kati ya maofisa hao, wapo wenye shahada katika sayansi ya kijeshi, usafiri wa anga, uhandisi wa ndege na mifumo yake, ulinzi na menejimenti ya kijeshi.

Katika hafla hiyo pia baadhi ya maofisa waliofanya vizuri kwenye mafunzo walizawadiwa, ambao ni Frank Wambura, Said Said, Yohana Charles, Kelvin Rafael, Emmanuel Petro na Anatoria Ndagile. 

Mkuu wa TMA alisema waliotunukiwa kamisheni wana elimu ya stashahada ya uzamili (1), shahada ya kwanza (24), stashahada (1), cheti (1) na kidato cha sita (101). Alisema ofisa aliyevishwa bawa ana shahada mbili.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alimwapisha Balozi Wilbert Ibuge kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles