Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Agosti 7, imetupilia mbali maombi ya dhamana ya mfanyabiashara Manji baada ya mawakili wake kukubaliana na mapingamizi ya Jamhuri.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Isaya Arufani, baada ya kukubaliana na hoja ya pande zote mbili ambapo amesema mahakama hiyo haina haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo.
Aidha, Jaji Arufani amesema mleta maombi hatowakilishwa tena na Wakili Peter Kibatala kama alivyowasilisha maombi yake, badala yake atawakiliswa na Wakili Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Seni Malimi.