28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Manji amwengua Bin Kleb Yanga

Yusuf Manji
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji

NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Yanga chini ya Mwenyekiti wake, Yusuf Manji, umemwengua madarakani Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Abdallah Bin Kleb huku ikiunda upya Kamati ya Utendaji.

Manji na Makamu wake, Clement Sanga walifikia uamuzi huo na kamati zote zilizoko chini ya Kamati ya Utendaji  zitavunjwa kuanzia Julai 30 huku kamati mpya zikianza kazi Agasti mosi mwaka huu.

Akitangaza wajumbe wapya wa Kamati ya Utendaji mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alimtaja Abubakar Rajab kuwa ndiye atakayeshughulikia Mradi wa Jangwani City, Sam Mapande (Sheria na Utawala), George Fumbuka (Uundwaji wa Shirika), Waziri Barnabas (Vibali vya Hatimiliki na Mahusiano na Wafadhili), Abbas Tarimba (Mipango na Uratibu).

Wengine ni Isaac Chanji na Seif Ahmed ‘Magari’ watakaoiongoza Kamati ya Uendelezaji wa Michezo, Musa Katabalo akiongoza Kamati ya Mauzo ya Bidhaa, Mohamed Bhinda Kamati ya Ustawishaji wa Matawi, David Ndeketela Kamati ya Uongezaji wa Wanachama na Mohamed Nyenge Kamati ya Utangazaji wa Habari, Taarifa na Matangazo.

Njovu aliwataja Wajumbe wa Kamati ya Utendaji iliyoundwa upya kusimamia kamati ndogondogo kuwa ni Sam Mapande atakayeongoza Kamati ya Maadili, ambaye pia ataongoza Kamati ya Nidhamu na Kamati ya Uchaguzi wakati Kamati ya Uchumi na Fedha itaongozwa na George Fumbuka na Waziri Barnabas.

Wengine ni Seif Ahmed ‘Magari’ na Isaac Chanji (Kamati ya Mashindano), ambao pia wataongoza Kamati ya Soka la Vijana na Wanawake na Kamati ya Ufundi.

“Tunaomba ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha Yanga inapiga hatua mbele na inafanikiwa katika kufikia malengo yake ya maendeleo ya muda mfupi na mrefu kwa manufaa ya klabu, timu na wana Yanga popote walipo duniani,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles