26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

Mane: Nataka mabao 30

SAFARI hii, mshambuliaji wa Liverpool raia wa Senegal, Sadio Mane, amejiwekea malengo ya kuzipasia nyavu mara 30 baada ya kuvurunda msimu uliopita.

Liver ikiwa imeshachezea mechi tatu, Mane amefunga bao moja lakini msimu uliopita haukuwa mzuri kwake kwani alicheka na nyavu mara 16 pekee katika mechi 48.

“Nilisikitishwa na kilichotokea msimu uliopita, naamini ningeweza kufanya vizuri zaidi…” amesema Mane aliyesajiliwa mwaka 2016 akitokea Southampton, ambapo usajili wake uligharimu Pauni milioni 34.

Katika msimu wake wa kwanza Anfield, alifunga mabao 13, kisha akaweka kambani mabao 20 au zaidi kwa misimu mitatu mfululizo, kabla ya kiwango chake kushuka ghafla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,621FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles