29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Messi kurudi Barca?

KWA mujibu wa lejendari wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Juan Roman Riquelme, Lionel Messi ataipa PSG taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kisha kurejea Camp Nou kumalizia soka lake.

“Kama PSG hawatakuwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa wakiwa na Messi, basi itakuwa imekula kwao. Messi atawapa ubingwa na kisha kwenda kustaafu akiwa na Barcelona,” amesema Riquelme aliyewahi kutamba na Villarreal.

Wakati huo huo, mabosi wa Barca wamempa sharti kocha wao, Ronald Koeman, wakimwambia atafukuzwa endapo atashindwa kuipa timu hiyo ubingwa wa La Liga msimu huu.

Koeman (58), anapewa sharti hilo huku akiwa ameshaiwezesha Barca kushinda mechi mbili za sare moja kati ya tatu za msimu huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles