22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Manchester kuvunja rekodi kwa Verratti

Marco Verratti
Marco Verratti

LONDON, ENGLAND

KLABU ya soka ya Manchester United ipo katika mipango ya kupata saini ya mchezaji wa kimataifa wa nchini Italia na kiungo wa timu ya Paris Saint Germain (PSG), Marc Verratti, ili kutua katika dimba la Old Trafford.

Kocha mpya wa klabu hiyo, Jose Mourinho, amepanga kukitengeneza kikosi mahiri cha timu hiyo ambacho mara ya mwisho  kuwa bora ilikuwa mwaka 2013 ambapo ilimaliza Ligi Kuu England ikiwa nafasi ya tano.

Kwa mujibu wa mtandao wa Corriere dello lilidai kuwa United ilitenga Euro 100 ili kuipata saini ya kiungo huyo wa zamani wa timu ya Inter Milan.

Kukamilika kwa usajili huo kunaweza kuvunja rekodi ya klabu hiyo ya Euro milioni 75 ya usajili wa Angel Di Maria mwaka 2014.

Pia kiungo huyo kama atatua Old Trafford anaweza kuungana na mchezaji wa zamani wa PSG, Zlatan Ibrahimic ambaye yupo mbioni kutua kwenye timu hiyo. Nyota huyo ambaye ni nahodha wa  timu ya taifa ya Sweden, alitangaza hivi karibuni kuondoka klabu ya PSG.

Kipindi hiki cha usajili kinaweza kuwa muhimu kwa Mourinho ambaye tayari amemaliza usajili wa Eric Bailly kutoka Villarreal huku akiwa mbioni kuipata saini ya wachezaji wawili kutoka klabu ya Juventus, Alvaro Morata na Paul Pogba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles