24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mamia wajitokeza kumzika Mez B

jeneza(1)NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA
MAMIA ya mashabiki na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, jana walijitokeza kuupumzisha mwili wa msanii, Moses Bushangama ‘Mez B’, katika makaburi ya Wahanga wa Treni, Mailimbili mkoani hapa.
Akizungumza wakati wa kuuaga mwili huo, mama wa marehemu, Mchungaji Mary Katambi, aliwataka vijana kumrudia Mungu.
“Mwanangu aliuona uwepo wa Mungu, nilikuwa nikimsihi kuokoka na kumrudia Mungu na alikuwa akinijibu itafika wakati mimi wa yeye kufanya hivyo,” alisema Mary.
Upande wake msanii wa kundi la Chemba Squad, Noorah alisema wamesikitika kumpoteza Mez B kwani alikuwa ni msanii anayependa ushirikiano na pengo lake halitaweza kuzibika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles