24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kinana:Tamasha la Pasaka liombee amani Tanzania

kinanaNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ametoa wito kwa waandaaji wa Tamasha la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions kuongeza ufanisi kwa kuongeza chachu kwa waimbaji kuiombea amani Tanzania hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kinana sambamba na hilo kwa pamoja tuiombee nchi yetu umoja, amani, mshikamano ambako tamasha hilo litumike kumuomba Mungu kufanikisha umoja kwa Watanzania ulioasisiwa na baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere.
Kinana alitumia fursa hiyo kuwatakia heri na fanaka Wakristo wote duniani heri na fanaka katika sherehe hizo ambazo ni kumbukumbu kubwa kwao ambayo haifanani na nyingine za kijamii.
Aidha Kinana alimpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama kwa kuwaunganisha Watanzania wa madhehebu mbalimbali na kuwa kitu kimoja na kudumisha mshikamano katika jamii.
Kinana alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa mashabiki na wapenzi wa tamasha hilo kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha mipangilio ya Msama katika kuisaidia jamii ya Watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles