28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mama wa 2pac afariki dunia

afeni-davisNEW YORK, MAREKANI

MAMA wa msanii wa zamani wa hip hop, marehemu Tupac Shakur, Afeni Davis, amefariki dunia juzi usiku kwa mshituko wa moyo.

Mama huyo amefariki nyumbani kwake mjini California baada ya kuugua ghafla, ambapo familia ilijaribu kumkimbiza katika hospitali ya karibu lakini alipoteza maisha kabla ya kufika.

Amefariki akiwa na umri wa miaka 69, hata hivyo kabla ya kifo chake alikuwa na mgogoro na mume wake kwa madai ya kutaka kugawana mali za zamani za 2pac na zile mpya ambazo ziliokotwa mwezi mmoja uliopita.

Mama huyo alikuwa maarufu sana baada ya 2pac kutoa wimbo wa kumsifia ambao ulikuwa unajulikana kwa jina la ‘Dear Mama’ ambao uliachiwa mwaka 1995.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles