WALTER MGULUCHUMA– KATAVI
MKAZI wa Kijiji cha Kanoge wilayani Mpanda Katavi,Emmanuel Kwizera (40), anatuhumiwa kutoroka na kuishi kinyumba binti yake wa kuzaa mwenye umri wa miaka 14.
Baba huyo alitoroka na binti yake, baada ya kutuhumiwa kumpatia ujauzito miaka mitano iliyopita.
Mama mzazi wa mtoto huyo, Mwajuma Ramadhani aliwambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuwa umefika wakati wa Serikali kumsaidia kumsaka mumewa ili afikishwe mbele ya vyombo vya dola.
Akizungumza kwa masikitio makubwa, Mwajuma alisema kitendo alichofanyiwa na mume wake, ni cha kulaniwa na jamii, kwani si cha kawaida hata kidogo kwenye jamii ya Watanzania .
Alisema mumewe Kwizera, wamezama naye watoto wanne ambao wote amewatelekeza kwake.
Akielezea mkasa wa mtoto wake kuolewa na baba yake, alisema alianza kuona mapenzi yake na mume wake siku hadi siku, yakipungua, huku mume wake akiwa na mapenzi zaidi kwa mtoto.
Hali hiyo ilianza kumshtua,ndipo alianza kuwafuatilia ili kujua kwanini baba amekuwa na mapenzi zaidi na mtoto kuliko yeye.
Alisema siku moja katika kufatilia, alikuta mume wake akiwa anamuuliza mtoto wake kuwa endapo kama atamzalisha mtoto wa kike atampa jina gani mtoto wake.
Alisema maneno hayo, aliyoyasikia yalizidi kumpa wasiwasi na kumfanya azidi kuwafutilia zaidi ili kujua ukweli wa mambo juu ya uhusiano uliopitiliza baina ya wawili hao.
Alisema siku moja, wakiwa nyumbani ghafla mume wake alitoweka na binti yake muda mrefu, akalazimika kuwatafuta.
“Baada ya kuwafuatilia vizuri, nilifanikiwa kuwafumania wakiwa wamelala pamoja kwenye jengo la banda la kuchomea tumbaku.
“Nilipiga yowe ili majirani wafike kuona kitendo hicho cha aibu, kwa kweli walifika wengi.
“Baada kufika eneo lile, walitushauri twende nyumbani kufanya kikao ambacho kilifanyika usiku kilimalizika usiku wa wanane, baada mume wangu kuomba msamaha, nilikubali kumsame kumsamehe,”alisema .
Alisema majirani waliokuwa kwenye kikao hicho cha usululishi, walifikia azimio, kuwa siku inayofuata mtoto apelekwe kituo cha afya Kanoge ili apimwe kama atakuwa na ujauzito na alipopimwa alibainika alikutwa na na mimba ya miezi minne .
Alisema wakati anataka kupeleka taarifa kwa uongozi wa Serikali ya kijiji, alipata maradhi na kulazwa kituo cha afya cha Kanoge, aliporusiwa kurudi nyumbani kwake alikuta mume wake na mtoto wameondoka.