27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Jafo aagiza shule ipewe jina la DC Mwegelo

 MWANDISHI WETU– KISARAWE

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo ameagiza shule ya bweni ya sekondari ya wasichana inayoendelea kujengwa Kijiji cha Mhaga,ipewe jina la Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Alisema kutokana na nguvu kubwa ya utendaji kazi wa mkuu wilaya, ameshawishika kuona shule hiyo, ikipewa jina la kiongozi, huku akimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Mussa Gama na maofisa elimu kuhakikisha wanalisimamia hilo.

Waziri Jafo, alitoa maagizo hayo mwishoni mwa wiki wilayani humo, akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo kubwa ya wasichana, inayojengwa chini ya usimamizi wa Mwegelo.

“Mkurugenzi ,ofisa elimu wilaya, nawaagiza shule kuazia sasa hakikisheni mnaipa jina la Mkuu wa Wilaya, Jokate Mwegelo, ni kiongozi wa mfano katika wakuu wangu wote wa wilaya, anafanya kazi kubwa na ni mbunifu, shule hii ikipewa jina lake ni heshima kubwa mno.

“Wilaya ya Kisarawe wapita viongozi wengi, hajawahi kuona kiongozi mchapa kazi kama huyu, namtakia heri katika kazi yake na Mungu ampandishe kutoka hapa alipo,”alisema.

Wakati huo huo, Waziri Jafo alifichua siri ya kuchapa kazi baada ya kusema baada ya kuteuliwa,yeye waziri na Mbunge wa Kisarawe, alimwita ofisini kwake na kumweleza changamoto za susani nyanja ya elimu.

Alisema moja ya moja ya maelekezo yake, ilikuwa kusimamia suala zima la kuinua kiwango cha elimu na kuja na mpango mkakati.

Alisema baada ya mazungumzo hayo, ndiyo ukaja mkakati wa kauli mbiu ya Tokomeza ziro kisarawe.

“Nataka kuwaeleza ndugu zangu wanakisarawe, Jokate baada ya kikao chetu pale ofisni kwa kweli matunda yake ndio haya mnayoyaona,”alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Jafo alisema ameridhishwa na ubora wa ujenzi wa shule hiyo pamoja na gharama zilizotumika nakwamba hakuna shaka kabisa mafundi wamefanya kazi Yao vizuri Sana.

Kwau pande wake, Mwegelo alisema shule hiyo ni ya kwaza kwa maana ya bweni kwa watoto wa kike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles