24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

IGP: Vitendo vya unyang’anyi wa silaha vimepungua

 LEONARD MANG’OHA– DAR ES SALAAM

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, amesema vitendo vya harifu, ikiwamo utekaji na uyanganyi wa kutumia silaha mkoani Singida, vimepungua kwa kiasi kikubwa, ikilinganishwa na awali.

Alitoa kauli hiyo mkoani Singida jana, ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mikoa mbalimbali kungalia jinsi walivyojitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

IGP Sirro alisema mbali na kupungua kwa matukio ya utekaji na unyang’anyi wa kutumia silaha pia matukio ya ajali za barabarani mkoani humo yamepungua kwa asilimia 50.

“Leo (jana), kubwa napita mikoa iliyobaki kuona utayari wao ukoje kwa uchaguzi ambao sasa tunajiandaa nao. Lakini kimsingi nilikuwa naangalia ajali katika mkoa wa Singida kwa miezi hii mitano zimepungua kwa asilimia 50, utekaji na unyang’anti wa kutumia silaha wana muda mrefu haujatokea katika mkoa wa Singida,” alisema IGP Sirro.

Sirro alilipongeza jeshi la polisi mkoani humo na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kwa ushirikiano ambao umesaidia kupunguza vitendo hivyo.

Katika hatua nyingine, aliwataka watu wanaoachiwa huru kwa msamaha wa rais kuhakikisha wanaachana na vitendo vya uharifu akidai kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya uharifu hasa katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha na Mwanza kila rais anapotoa msamaha kwa wafungwa mbalimbali.

Alisema kitendo cha wafungwa wanaoachiwa kwa msamaha wa rais kurudia kufanya vitendo hivyo kunaibua hasira miongoni mwa wananchi jambo linalosababisha kuchukua uamuzi wa kuwapiga na kuwadhuru.

“Niwaombe ndugu zangu wanaopata hii misamaha ni vizuri ukakaa na kujiuliza na kuona kwamba ni msaada umepata huna sababu ya kurudumia kufanya uharifu.

“Na mara nyingi wanaporudia kufanya uharifu wanapoteza maisha, mara nyingi wanakutana na polisi wanapoteza maisha. Na sisi polisi hatupo kwa ajili ile, lakini tunapopambana na hawa wanaotumia silaha hakuna namna ni suala la kuwahiana,” alisema IGP Sirro.

Aliziomba familia za wayu wanaopata msamaha wa rais kuhakikisha wanakaa nao na kuwaeleza namna bora ya kuishi asipoelewa asiilaumu serikali na kwamba jeshi hilo na mtu yeyote anayejihusisha na unyang’anti wa kutumia silaha. Alisema wanataka masuala ya utekaji wa magari nabunyang’anti wa kutumia silaha nchini uwe historia hivyo wanaoendelea kulazimisha wasiilaumu serikali.

Kuhusu uchaguzi mkuu, alisema tatami jeshi hilo limepeleka polisi kata katika kata zote nchini ili kuhakikisha wanatoa wanatoa elimu kwa jamii kuhusu masuala mbalimbali, ikiwamo matumizi ya dawa za kulevya.

Alisema kati ya Januari na Mei, mwaka huu, mkoa ya jinai yaliyoripotiwa ni 175 ikilingalishwa na makosa 347 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka uliopita yakiwa yamepungua kwa makosa 172 sawa na asilimia 50, huku makosa mdogo yakipungua kutoa 4,762 mwaka jana hadi 4,728 mwaka huu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles