23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mama akutwa na kuku sehemu za siri Kigoma, Mganga Mkuu athibitisha

Na Mwandishi Wetu

Mwanamke mmoja Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, amejifungua kuku katika kituo cha Afya Uvinza baada ya kufika kituoni hapo akidai anapata maumivu ya tumbo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Simon Chacha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema tukio hilo limetokea leo asubuhi Jumapili Desemba 6, 2020 baada ya mama huyo kufika katika kituo cha afya akiwa na Mumewe akisumbuliwa na maumivu ya tumbo.

“Baada ya muda wauguzi walitoa kuku katika sehemu ya uzazi ya Mama huyo ambapo hakuna damu zilizoendelea kutoka zaidi ya uchafu tu unaotoa harufu mbaya,”amesema Chacha.

Amesema tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina kwa kuwa vipimo vinaonyesha mama huyo hakuwa na dalili yoyote ya ujauzito na haoneshi kama alikuwa na ujauzito na baada ya kutolewa kuku huyo ameendelea kutoa harufu mbaya katika sehemu hiyo ya uzazi na alikuwa na homa.

Hata hivyo Chacha, amemuagiza Mganga Mfawidhi ampeleke hospitali ya Rufaa Maweni kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi.

“Mama huyu haoneshi dalili zozote ya kwamba alikuwa na ujauzito cha kushangaza zaidi kiumbe hicho hakiusiani na mfuko wa uzazi isipokuwa baada ya vipimo imeonekana mama huyo ana uvimbe kwenye kizazi mpaka sasa tumewasiliana na vyombo vya usalama kufuatilia tukio hilo”, amesema Chacha.

Kwa upande wake Mama huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, amesema alianza kujisikia maumivu tumboni na hakuwa na dalili zozote za mtu mwenye mimba ameshangaa baada ya kufika Hospitali hapo kutolewa kuku tumboni mwake jambo ambalo pia limemuogopesha.

 Taarifa zisizo rasmi zinasema kwamba mama huyo aliingiziwa kuku huyo na Mganga wa kienyeji.

Nao baadhi ya Wananchi Wilayani humo akiwemo Riziki Mbonabucha wamesema tukio hilo limewashangaza sana maana halijawahi kutokea katika Wilaya ya Uvinza na kama kuna mtu anahusika na kumfanyia kitendo hicho mwenzake achukuliwe hatua ili iwe fundisho.

Amesema kazi ya Waganga wa kienyeji ni kuwaondolea Wananchi matatizo na sio kuwaongezea matatizo anashangaa kuona Mganga huyo aliyekosa roho ya huruma kukubali kumuwekea mwanamke kuku tumboni ni unyama unaohitajika kukomeshwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles