Bamako, Mali
Nchi ya Mali imevuliwa uanachama wa Jumuiya ya Africa Magharibi Ecowas baada ya kufanyika mapinduzi ya awamu ya pili ya kijeshi nchini humo wiki iliyopita.
Kiongozi wa mapinduzi na ambaye sasa ni Kanali Assimi Goïta, alihudhuria mkutano katika mji mkuu wa Ghana, Accra.
Waziri wa mambo ya nje nchini Ghana Shirley Ayorkor Botchwey, alisema jumuiya hiyo imeitolea wito Mali kumteua Waziri Mkuu mpya raia mara moja, ili kuheshimu kipindi cha mpito cha miezi 18 na kufanya uchaguzi wa rais mwezi Februari.
Ghana ilisema utulivu wa Mali ni muhimu ili Afrika Magharibi iweze kudhibiti harakati za ugaidi katika kanda hiyo.
Kanal Goïta alinyakua mamlaka baada ya kuamuru kukamatwa kwa Rais Bah Ndaw na waziri mkuu Moctar Ouane.