29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Simulizi ya Priscilla alivyotoa mimba kwa majivu, kitunguu swaumu

*Marie Stopes na mkakati wa usambazaji elimu afya ya uzazi nchini

Na Esther Mbussi, Mtanzania Digital

Afya ya uzazi ni muhimu kwa vijana kwani inawajengea uelewa wa jinsi ambavyo wanaweza kupanga na kuchagua namna bora ya familia zao na jinsi watakavyowalea.

Licha ya kuwajengea uelewa, elimu hiyo afya uzazi ni muhimu kwao kwani pia itafunza mambo mbalimbali yahusuyo afya ya uzazi na magonjwa ya ngoni kwa vijana ambayo yamekuwa yakiwasumbua vijana wengi.

Ni kutokana na changamoto hizo, Shirika la Marie Stopes Tanzania liliamua kijikita katika kutoa elimu ya afyaa ya uzazi kwa watu wote ili kila mtu afurahie maisha na kuona kuwa dunia ni sehemu salama ya kuishi kwani kupanga ni kuchagua.

Lakini pamoja na jitihada hizo za kutoa elimu ya afya ya uzazi, bado kuna baadhi ya maeneo kuna changamoto ambapo elimu sahihi haijawafikia vijana hususani wanafunzi wa kike ambao wamekuwa wakipata ujauzito na kutoa kwa njia mbalimbali zisizo salama ambazo wamekuwa wakijadiliana bila kushirikisha wataalamu.

Priscila Ortmund (19), ni miongoni mwa wanafunzi wa kike ambao walipata ujauzito na kuutoa kwa njia zisizo salama na hatimaye kupoteza kizazi.

Akisimulia mkasa wake ambao ulisababisha yeye kuacha shule kutokana na kuugua kwa muda mrefu baada ya kutoa mimba kwa kutumia majivu, majani ya chai na kitunguu swaumu anasema katika vitu ambayo anajuta katika maisha yake ni kufanya kitendo hicho ambacho kilimsababishia maumivu makubwa na kumwachia makovu maishani.

“Nilikuwa nasoma shule kijijini (Iringa) na nilikuwa kidato cha tatu wakati nimepata ujauzito ambao nilipewa na mwanafunzi mwenzangu lakini yeye alikuwa kidato cha nne. Nikamwambia rafiki yangu Anet na yeye akamwambia mwanafunzi mwenzetu mwingine ndiye akaja na ushauri uliosababisha mimi kuacha shule.

“Alinishauri nichukue majivu na majani ya chai nichanganye na maji halafu punge za vitunguu swaumu niingize kwenye kizazi kwa kutumia vidole nikaweka. Alisema alifundishwa na dada yake (msichana wa kazi) ambaye aliwahi kufanya hivyo alipopata ujauzito na ukatoka,” anasema Priscilla.

Baada ya kunywa mchanganyiko huo kwa siku mbili mfululizo, Priscilla anasema alianza kusikia tumbo linamuuma kama kuna mtu anakoroga kitu tumboni akajipa moja ndiyo mimba inaharibika hivyo kavumilia ili itoke kabisa aendelee na masomo lakini pia wazazi na walimu wake wasifahamu lolote kuhusu jambo hilo.

“Siku ya pili tumbo likaanza kuniuma sana kiasi kwamba nilishindwa kujizuia walimu na wanafunzi wenzangu wakaanza kuulizana nini tatizo ndipo ikabidi niseme ukweli nikamtaja na Anet lakini alikataa kuwa alinipa ushauri ule.

“Nyumbani nako mama akasema nipewe dawa za kutuliza maumivu kwani hakukuwa naa fedha za kunipeleka hospitali. Baada ya wiki mbili nikaanza kuona uchafu unatoka ukeni ukiwa na harufu kali na tumbo halikuacha kuuma, nikamwambia mama akasema hii sasa hatari ndipo nikapelekwa hospitali ikagundulika mimba ilikuwa imeharibika na kizazi kilikuwa kinalika kwa kuoza na sehemu za karibu na kizazi.

“Kwa hiyo ikabidi nifanyiwe upasuaji sasa sijui waliondoa kizazi au walisafisha tu lakini mama aliniambia kwa sababu ya kuharakia maisha sitaweza kuzaa tena,” anasema

Priscilla ni mmoja kati ya wasichana wengi ambao hawana elimu ya afya ya uzazi. Kuulingana na simulizi yake hiyo angekuwa na elimu hiyo asingepata ujauzito wa bila malengo lakini pia asingetumia njia zisizo salama kuharibu ujauzito wake.

Dk. Elias Kweyamba ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, anashauri wasichana wanaopata ujauzito wasinyanyapaliwe bali wapewe huduma stahiki na kikubwa zaidi elimu ya afya ya uzazi.

Anazungumzia utoaji wa mimba isiyo salama anasema mara nyingi hufanywa na watu wasio wataalamu au kufanywa kwenye mazingira yasiyo salama kama ilivyotokea kwa Priscilla ambaye alijaribu kuharibu mimba bila kujua kwanza kama mimba hiyo kama inamhatarishia maisha yeye au mtoto aliye tumboni.

“Utoaji wa mimba usio salama hufanywa na watu wasio wataalamu ili kujipatia fedha kutoka kwa mhusika ambaye hauhitaji ujauzito huo kwa wakati huo kwa kuwa hakujipanga, ila utoaji salama hufanywa na wataalamu na kwa sababu maalumu kama vile mama mwenye kifafa cha mimba haijalishi ni ya muda gani lazima umtoe, mimba iliyoharibika au kutoka damu sana hapo lazima umtoe mama mjamzito mimba ili kuojoa maisha yake,” anasema.

Anataja takwimu kuwa watu milioni 56 duniani hutoa mimba ambapo kati ya hizo 25,000 huwa si salama na wengi wao kati ya asilimia 98 ni katika nchi zilizoendelea ikiwa 3,000,000 ni wasichana kati ya miaka 15-19.

“Wengine milioni 6.9 wanapata tiba ya madhara ya utoaji mimba ambayo si salama huku asilimia 40 hawapati tiba na milioni saba hupata tatizo la kudumu na mara nyingi asilimia 91 ya vifo hivyo hutokea Afrika na Asia,” anasema Dk. Kweyamba.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016 kwa Afrika Mashariki mimba milioni moja zisizotarajiwa sawa na asilimia 39 hutolewa kwa njia zisizo salama, watu 405,000 kila mwaka walitoa mimba ambapo asilimia 40 walihitaji tiba lakini hawakupata tiba stahili.

“Mara nyingi nchi ambazo wanawake hawako vizuri kiuchuni huwa na tatizo la utoaji mimba usio salama.

“Ili kupunguza tatizo la utoaji mimba usio salama ni kutoa huduma za kisaikolojia, kuondoa unyanyapaa kwa wajawazito na watu kubeba mimba kwa mpango,” anasema Dk. Kweyamba

Nini hufanywa na Marie Stopes kusaidia tatizo hilo?

Shirika la Marie Stopes lilianzishwa mwaka 1989 nchini kwa lengo la kutoa elimu ya afya ya uzazi ambapo hadi sasa ina vituo tisa na zahanati nane zinazotoa huduma hiyo nchini.

Huduma zinazotolewa ni pamoja na uzazi wa mpango, uchunguzi wa afya, afya ya mama na mtoto, utunzaji wa baada ya kutoa mimba salama, uchunguzi wa saratani ya kizazi, huduma ya msingi ya afya, huduma ya uzazi na huduma za uchunguzi wa magonjwa ya zinaa na Virusi Vya Ukimwi (VVU), uchunguzi wa malaria na matibabu, chanjo na ukaguzi wa afya ya mtoto.

Marie Stopes pia inawawezesha vijana kwa kuwashirikisha katika mawasiliano rafiki na shughuli za vijana na kuelimisha kuhusu afya ya uzazi.

Lengo ni kutoa huduma haswa katika maeneo magumu kufikika hususani vijijini na makazi duni ya mijini kupitia timu za ufikiaji wa kliniki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles