29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wanafunzi watekwa nyara Nigeria

Niger, Nigeria

Jeshi la polisi nchini Nigeria imetoa ripoti ya kutekwa nyara wanafunzi wa shule moja ya kiislamu iliyopo jimbo la Niger katikati mwa nchi hiyo.

Katika ripoti hiyo imesema watu wenye silaha walifanya shambulizi shuleni hapo na kuwateka wanafunzi huku bado idadi kamili haijajulikana ya watoto waliotekwa nyara.

Msemaji wa polisi ya jimbo Niger Waisu Abiodun amesema washambuliaji waliwasili eneo la shule kwa pikipiki na kuanza kufyetua hovyo risasi zilizosababisha kifo cha mkazi mmoja na kumjeruhi mwingine.

Mmoja wa maafisa wa shule hiyo amesema awali washambuliaji waliwateka nyara watoto 100 lakini baadaye waliwarudisha wale wenye umri kati ya miaka 4 hadi 12.

Kwa muda mrefu sasa makundi ya watu wenye silaha yanaendesha ukatili kaskazini magharibi mwa Nigeria kwa kufanya uporaji wa mali, mifugo na kuteka watu nyara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles