26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mali yaondolewa Uachama na AU

Bamako, Mali

Nchi ya Mali imeondolewa kwa muda uanachama wa Muungano wa Afrika kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya wiki iliyopita, yakiwa ya awamu ya pili katika kipindi cha miezi tisa.

Mapinduzi ya kwanza yalifanyika mwezi Agosti mwaka 2020 yaliyofuatiwa na mapinduzi ya kijeshi, lakini nchi hiyo ilirejea katika hali ya utulivu baada ya kutangazwa kwa viongozi wa kiraia kuongoza serikali ya mpito.

Katika taarifa yake AU imetoa wito wa kurejeshwa mamlakani kwa serikali ya kiraia ikisema kuwa haitasita kuiwekea vikwazo na hatua nyingine za adhabu iwapo wanajeshi hawataamrishwa kurudi katika kambi zao.

Jumatatu, viongozi wa Jumuiya ya Afrika Magharibi – Ecowas pia waliiondoa nchi ya Mali kwa muda katika uanachama wa jumuiya hiyo, na kuitolea wito serikali ya kijeshi kuheshimu kipindi cha mpito cha miezi 18 kuelekea uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi februari mwaka ujao.

Kanali Assimi Goita, ambaye aliongoza mapinduzi, aliteuliwa kama rais wa mpito na mahakama ya kikatiba ya nchi hiyo siku nne zilizopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles