23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Jenerali Wamala amshukuru Mungu dhidi ya shambulio la risasi

Kampala,Uganda

Waziri na Jenerali wa Uganda Katumba Wamala ametoa shukrani zake kufuatia shambulio la kupigwa risasi yeye Pamoja na binti yake lililotokea siku ya Jumanne asubuhi Juni 1, 2021.

Katika ujumbe alioutoa katika video fupi iliyorekodiwa katika Hospitali ya Medipal, Katumba ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amesema mungu amempa nafasi ya pili na atakuwa vyema.

Pia ameongezea na kusema hana majeraha mabaya, ni mikono tu na yupo na madaktari na wanafanya kila liwezekanalo kurudisha hali yake sawa na amewaomba wananchi kumuombea.

Hata hivyo katika shambulio hilo binti yake Wamala Brenda Nantongo, na dereva waliuawa katika shambulio lililofanywa na wanaume wanne ambao walikuwa kwenye pikipiki.

‘’Nimenusurika, lakini binti yangu Brenda Nantongo Katumba na dereva wangu Haruna walikufa katika eneo la tukio. Sijui sababu ya shambulio hili. Hapakuwa na sababu ya kumaliza maisha ya watu wasio na hatia. Roho zao zipumzike kwa amani’, ni ujumbe wake aliouandiika  Jenerali Wamala kupitia ukurasa wake wamtandao wa kijamii Twitter.

Mkuu wa majeshi ya Uganda David Muhoozi alikuwa mmoja wa maafisa wa jeshi waliofika kwenye eneo la tukio mara baada ya kutokea kwa shambulio hilo, ambalo limelaaniwa vikali na Rais Yoweri Museveni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles