29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Shirika la MSF yatoa ripoti ya Mlipuko wa magonjwa Kongo

Kinshasa, Kongo

Shirika la Medecins Sans Frontieres (MSF) limetoa ripoti ya tishio la ugonjwa wa mlipuko wa kuhara kufuatiwa ukosefu wa maji safi na salama katika mji wa Goma uliopata maafa ya mlipuko wa Volkano ndani ya Nchi ya Kidemokrasia ya Kongo.

Karibu watu 500,000 huko Goma wameachwa bila maji safi na salama ya kunywa baada ya mlipuko wa volkeno wiki mbili zilizopita.

Pia Shirika la Médecins Sans Frontières limesema kuna haja ya kuhakikisha watu wa mji wa Goma wamepata maji safi na salama kwaajili ya matumizi yao ya kijamii.

Hifadhi na mabomba yaliharibiwa baada ya mlipuko wa volkano uliotokea katika mlima wa Nyiragongo ulipolipuka Mei 22, 2021 huku mamia ya maelfu ya watu bado hawajaweza kurejea katika nyumba zao.

Mkuu wa utoaji msaada kupia shirika la MSF, Magali Roudaun alisema wanatoa msaada kwa mahitaji ya dharura kwa watu waliolazimika kuhama makazi yao, lakini haitoshi. huko DRC.

“Tunahitaji msaada wa dharura kutoka kwa mashirika mengine ya kutoa misaada ili kusaidia watu”, alisema Mkuu wa MSF, Magali.s

Shirika la MSF limesema timu yake ilikuwa inatoa huduma za matibabu katika mji uliokaribu wa Sake, mbapo kati ya watu 100,000 na 180,000 wamekusanyika makanisani, shuleni, misikitini na mitaani.

Shirika la Umoja wa Mataifa UN limesema kuwa Mlima Nyiragongo, kilomita 10 kutoka mji wa Goma, ulilipuka na kusababisha mtirirko lava siku 10 zilizopita, na kupelekea mauaji ya watu 32.

Kumekuwa na mitetemeko mingi nchini humo tangu tukio hilo .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles