29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

MALEMA ATAKA KISWAHILI KITUMIKE AFRIKA

 

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI


Kiongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini, Julius Malema, ametoa wito wa kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya kuliunganisha bara Afrika.

Mbali ya hilo, ametaka kupunguzwa kwa mipaka ndani ya bara, uwapo wa sarafu moja na Umoja wa Mataifa ya Afrika wenye Bunge na rais mmoja.

Katika mkutano na wanahabari juzi aliouitisha kuzungumzia masuala mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, Kiongozi huyo wa Chama cha Wapigania Uhuru wa Kiuchumi (EFF) alisema; “Tunatakiwa tuanzishe lugha itakayotumiwa na kuunganisha wengi barani Afrika. Mfano mzuri ni Kiswahili, kinaweza kutumika kufanikisha hilo.”

Wazo la kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya bara la Afrika limekwa likizungumziwa kwa miaka mingi, lakini ni nchi chache zilizotilia uzito pendekezo hilo.

Kiswahili ni moja ya lugha rasmi za Umoja wa Afrikia na ni lugha rasmi nchini Kenya, Tanzania na Rwanda na ina wazungumzaji zaidi ya milioni 100.

Lugha hiyo pia inazungumzwa nchini Burundi, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mbali ya kuhimiza lugha yenye kuwaunganisha Waafrika, Malema alisema; “Tunahitaji bara lenye mipaka michache, tunahitaji sarafu moja, Bunge moja na rais mmoja wa kutuunganisha.

“Tunahitaji Umoja wa Mataifa ya Afrika. Tunahitaji Afrika moja. Lakini kufanikisha hili, Afrika inahitaji lugha moja itakayounganisha watu,” alisema.

Hata hivyo, lugha za Afrika huwa hazipewi uzito badala yake lugha za kigeni kama Kiingereza, Kifaransa na nyinginezo zimekuwa zikipendelewa katika mataifa mengi.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles