Ferdnanda Mbamila, Dar es Salaam
Kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake, watoto na wakimbizi (WLAC), katika kipindi cha miaka 30 kimewezesha makundi hayo 92,491 kupata haki kupitia msaada wa sheria.
Kesi zilizoripotiwa zaidi Kwa kipindi hicho ni ndoa, ardhi, mirathi na matunzo ya watoto.
Wakili wa Kituo hicho, Theodorothia Muhulo amesema awali kulikuwa na mabadiliko makubwa ya uelewa wa wanawake kuhusu haki zao kati ya mwaka 2009 na 2018.
Amesema kwa wakati huo idadi ya wanawake wanaodai haki zao katika kesi za ndoa walikua wakiondoka katika ndoa.
“Idadi iliongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo wanawake walikua wakiondoka katika ndoa bila kudai mchango wao wa mali zilizopatikana wakati wa ndoa,” amesema Theodorosi.