Na Grace Shitundu
WAKATI makontena 20 yenye samani za shule ambayo yanadaiwa kuwa ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yakipigwa mnada kwa mara ya tatu jana, wanunuzi wameshindwa kufika bei.
Makontena hayo ambayo yanapigwa mnada na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart kwa idhini ya Mamlaka ya Mapato nchini(TRA) yalinadiwa jana katika ghala la Dar es Salaam Inland Container Deport(DICD) eneo la bandari Kurasini.
Kontena moja tu lenye namba 3200018 ndilo lililonekana kugombewa baada ya wanunuzi kuweka dau la kuanzia milioni 15 hadi 40 tofauti na makontena mengine ambayo dau lilikuwa ni kuanzia milioni tano na 18.
Mnada huo ambao ulianza takribani saa 4:16 pamoja  na kuwepo kwa makontena hayo ambayo yanadaiwa kuwa ya Makonda pia kulikuwa na makontena mengine ambayo yalikuwa na vifaa vingine vilivyokuwa vikiuzwa kama matrekta, magari na vifaa vya kilimo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevera alisema katika mnada huo wamefanya mnada wa vitu mbalimbali.
“Hatukuuza fanicha peke yake tumekuja kuuza vitu …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.