23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda: Sijaridhishwa na idadi ya watumishi hewa Dar

makondaNA HADIA KHAMIS,DAR ES SALAAM,

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hajaridhishwa na idadi ya watumishi hewa aliyopatiwa na maofisa utumishi.

Mbali na hilo, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwahoji maofisa utumishi wote wa mkoa huo,  kwani ndiyo wanaotoa taarifa zisizokuwa sahihi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini wake jana, Makonda alisema haiwezekani Mkoa wa Dar es salaam ulio na wajanja wengi na matapeli kuwa na wafanyakazi hewa 71 tu.

“Baada ya Rais kutoa agizo la kutaka kila mkoa utaje idadi ya watumishi hewa, niliunda tume ya kufanya uchunguzi, lakini kwa uchunguzi wa awali nililetewa idadi ya watu 71 kwa kweli hii idadi sikubaliani nayo.

“Inaonekana kuna watu wanatengeneza habari ili wajiongezee kipato hali ambayo wanatoa takwimu zisizo sahihi, kwa kuligundua hili nimeamua kufanya uchunguzi upya na kila siku idadi inaongezeka,”alisema Makonda.

Alisema kutokana na udanganyifu wa  takwimu zisizo sahihi, amewaagiza wakuu wa wilaya zote  kuacha shughuli zao na badala yake wafuatilie idadi ya watumishi hewa kwa kila wilaya.

Alisema amefanya mazungumzo na ofisi ya utumishi wa umma ili kupata idadi kamili ya watumishi wa serikali  walioko wilaya zote.

“Ofisi ya utumishi ndio ofisi inayojua idadi ya watumishi walioajiriwa, watatusaidia kujua ukweli baada ya hao wakuu wa wilaya kutoa taarifa za watumishi hewa ,”alisema  Makonda.

Alisema katika hatua nyingine za kupambana na watumishi hewa, tumepata mfumo wa malipo unaotambulisha watumishi wote ambao wanapokea mishahara kutoka serikalini.

Alisema Wilaya ya Kinondoni tayari watu 34 wamechukuliwa hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufunguliwa jalada tangu Aprili 8 mwaka huu.

Alisema amepata taarifa ya kuwapo watumishi ambao wamejifutia madeni baada ya kusikia uchunguzi unafanyika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles