24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa aongoza mamia kumzika Askofu Isuja

kassimNA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

WAZIRI Mkuu, Kasim Mjaliwa, jana aliwaongoza maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma pamoja na mikoa mingine katika mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma, marehemu Askofu Matias Isuja.

Askofu Isuja alifariki dunia wiki iliyopita katika Hospitali ya St. Gasper ya Itigi Manyoni mkoani Singida, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Marehemu Askofu Isuja ambaye alizikwa jana katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba  alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya utumbo.

Akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Rais Dk. John Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa  alisema wakati wa uhai wake, Askofu Isuja alitoa mchango mkubwa kwa jamii ya watu wa Dodoma na nje.

Alisema wakati wa uhai wake, Askofu Isuja alikuwa na mchango mkubwa katika kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo maji, elimu na afya.

Alisema kifo chake ni pigo kubwa kwa wakatoliki na wasio wakatoliki, kwani wakati wa  uhai wake hakubagua watu.

Alisema kinachotakiwa sasa ni kumwombea na kuendeleza yale yote mazuri ambayo aliyaanzisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles