28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

MAKONDA AZINDUA MFUMO UTAKAOWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO

Brighiter MasakiDAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Oktoba 9 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo kuwasilisha kero na changamoto walizonazo kwa kutumia simu ya mkononi na ujumbe wao kuwafikia watendaji kwa haraka na kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi jambo litakalosaidia kuokoa Muda na gharama za usafiri.

Makonda amesema ameamua kuanzisha mfumo huo baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wamekuwa wakifika kwenye ofisi za umma na kupewa majibu ya “Njoo Kesho” pasipokujua kuwa wamepoteza muda na nauli zao kufuata huduma.

Aidha Makonda amebainisha kuwa mfumo huo utakuwa ukipokea taarifa za malalamiko ya Watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata, Wilaya hadi Mkoa na taarifa zitawafikia Viongozi wote kuanzia Makonda mwenyewe, Mkuu wa Wilaya husika, Mkurugenzi, Katibu tawala na Mkuu wa idara.

Pia RC Makonda amewahimiza wananchi kutumia mfumo huo kueleza kero zote zinazowakabili ikiwemo Afya, Barabara, Elimu, Maji, Umeme, Miradi inayokwama pamoja na kutoa taarifa pindi wanapobaini uhalifu kwenye mtaa.

Jinsi kuwasilisha ujumbe andika neno DSM kisha eleza changamoto zako kisha tuma kwenye namba 11000 na ujumbe wako utapokelewa mara moja na kupewa mrejesho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles