Makampuni ya simu za mkononi yanavyosaidia ukuaji wa biashara ndogondogo na za kati (SMEs)

0
5616

Na Mwandishi wetu

Wafanyabiashara wadogo na wale wa kati (SMEs) hadi sasa wana uwezo wa kuchangia asilimia 35 ya pato la taifa (GDP) imefahamika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na kampuni ya kimataifa inayoshughulikia masuala ya simu za mkononi GSMA duniani imesema hivi sasa jumla ya asilimia 95 zinazojumhisha wafanyabiashara wadogo wadogo, wakati pamoja na wenye viwanda na kilimo nchini (SMEs), kwa ujumla wake wanachagia asilimia 35 ya pato la taifa.

Taarifa hiyo ambayo ipo katika mtandao wa GSMA, https://www.gsmaintelligence.com ilisema SMEs imekuwa kichocheo kikubwa cha uchumi na maendeleo nchini kwa sababu inajumuhisha sekta muhimu kama vile kilimo, usafirishaji na biashara mbalimbali.

Ilisema SMEs kwa kushirikiana na mashirika pamoja na makampuni mbalimbali yamesaidia kuleta mabadiliko chanya katika uchumi wa nchini kwa kuzalisha ajira, kukuza ubunifu, kutoa huduma na bidhaa kwa watu wa kipato cha chini.

Taarifa hiyo, iliendelea kusema ukuaji wa uchumi nchini unazingatia jinsia zote kwani wanawake, wanaume pamoja na vijana wanashiriki kikamilifu hivyo ni wazi kuwa SMEs itaisaidia Tanzania kukua kwa kiwango kikubwa kiuchumi hadi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Taarifa hiyo ilisema mbali na mafanikio hayo yanayotarajiwa kufikiwa 2025 ila kuna changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa kikwazo na kusababisha watu kukosa mitaji na kuzitaja baadhi ya changamoto kuwa ni masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijami.

Na kuongeza kuwa changamoto zingine zinazoikumba SMEs ni pamoja na ugumu wa kupata huduma za kifedha, kukosekana kwa huduma za intaneti iliyo imara na uhakika sehemu mbalimbali nchini hasa vijijini.

Taarifa hiyo, imezipongeza baadhi ya sekta binafsi kuwa bado zimekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha zinatafuta ufumbuzi wa changamoto hizo. Na kutoa mfano Kampuni ya Tigo Tanzania ni moja ya mifano ambapo imekuwa ikijishughulisha kuhakikisha inaboresha mazingira ya kibiashara ili kuhakikisha kuwa SMSe zinazidi kukua kila siku.

Taarifa hiyo, ilifafanua kuwa hivi karibuni Tigo ilitangaza kuzinduliwa kwa huduma ya intaneti ya ofisi, huduma ambayo imeletwa madhubuti kuhakikisha inaboresha upatikanaji wa inatenti katika SMEs. Huduma hiyo inatoa uwezo wa vifaa hadi 32 kwa wakati mmoja ambapo vifaa hivyo vitaweza kupata intaneti yenye kasi ya 4G+, na kuweza kutumia programu mbalimbali kupitia Microsoft 365.

Mbali na hilo, wamiliki wa biashara ndogo na za kati wanaweza kupata faida nyingine kwa kuwa mawakala wa huduma ya Tigo-Pesa. Kwa kufanya hivyo zitakuwa zinarahisisha ufanyaji wa biashara kwa kuungana na makampuni zaidi ya 70,000 ambayo yanakubali malipo kwa njia ya simu na kulipa ankara mbalimbali kupitia huduma ya Tigo Pesa na Wallet.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here