31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

NAIBU WAZIRI ELIMU AIPA RUNGU NACTE KUFUNGIA VYUO VINAVYOCHELEWESHA MATOKEO

Brighiter Masaki – DAR ES SALAAM.

NAIBU Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia William Ole-Nasha, ameliagiza Baraza la Taifa la Elimu na ufundi (NACTE) kuvifutia usajili vyuo vyote vinavyosajili wanafunzi bila kufata utaratibu.

Pia alitaka baraza hilo, kuvichukulia hatua kali vyuo ambavyo vinavyochelewesha matokeo ikiwa ni pamoja na kuvifungia.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea ofisi hizo, anasema kuwa Sheria zifuatwe ili vyuo visiwe vikwazo kwa wanafunzi kushindwa kusonga mbele.

“Inatakiwa kuangalia ubora wa wanafunzi kuna vyuo vinavyosajiliwa kiholela mwishoni mwanafunzi anakuja kugundua kuwa hana sifa, Ukigundua chuo kama hicho chukua hatua kali pamoja na kufuta usajili wa hicho chuo, hata kama nicha serikali hakikisheni vyuo vinachukuwa wanafunzi wenye sifa stahiki.

“Hakikisheni Orodha ya wanafunzi ambao hawajapata vyeti malizeni kwanza waliosajiliwa kwa mfumo wa Analogi mkimaliza anzeni na wadigital ili kusaidia kupunguza malalamiko kuwa mengi.

“Ucheleweshaji vyeti unaathiri wanafunzi wanafunzi pamoja na wazazi, kujenga mitaara mizuri ya kujiajiri mwenyewe na wanaopenda kuajiliwa waweze waajirike”amesema Ole Nasha.

Aidha Naibu Waziri Ole Nasha alisema kuwa wanafunzi wanashindwa kujisajili kwa kutokujuwa utaratibu, hivyo NACTE wanapaswa kutoa elimu kwa wanafunzi ili kujuwa jinsi ya kujiunga katika nafasi hizo na kujuwa jinsi ya kujisajili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles