27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAKAZI HOLELA YAMTISHA MBUNGE WAITARA

Na MWANDISHI WETU

MAKAZI holela ya wananchi yamemtisha Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), ambapo ameamua kuita wataalam kutoka Chuo cha Ardhi Morogoro ili kutoa elimu kwa wananchi, sambamba na kuwapimia makazi yao ili yaweze kutambulika rasmi.

Akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Mwembeni Kata ya Kitunda mwishoni mwa wiki, Waitara alitumia mkutano huo kuwataka  wananchi kuunga mkono mradi wa upimaji ardhi ambao upo katika eneo lao.

Alisema faida kubwa ya makazi yaliyopimwa na kutambuliwa rasmi ni pamoja na kuongezeka kwa thamani ya ardhi husika, kuondoa migogoro pamoja kuweka dhamana ya kuomba mkopo katika taasisi kubwa za fedha.

“Asilimia kubwa ya wananchi wa Jimbo la Ukonga wana ardhi lakini ni watu masikini, hivyo niwaombe tuchangamkie huu mradi wa upimaji makazi, leo hii kama una ardhi yako unataka kuiuza ipime kwanza ili thamani yake ipande mara tatu ya bei uliyotarajia.

““Jimbo la Ukonga lina makazi zaidi ya 20,000 lakini waliopima ardhi yao na kupata hati hawazidi 1,000, niwaombe tushirikiane kupima makazi yetu, leo hii ukiwa na ardhi lakini haijapimwa haiwezi kukusaidia, tuitumie ardhi  kujikwamua kiuchumi,” alisema Waitara.

Mbali na hilo, mbunge huyo aliwakumbusha wananchi umuhimu wa kufuatilia elimu ya watoto wao na kuachana na dhana kuwa serikali inatoa elimu bure huku akisisitiza kuwa hakuna muujiza wowote kwenye ufaulu wa mwanafunzi kama hakuna maandalizi ya kutosha.

Naye Mkufunzi na Mratibu wa Urasimishaji Makazi kutoka Chuo cha Ardhi Morogoro, Adolph Milunga alisema gharama ya upimaji inayotambuliwa na Serikali ni Sh 300,000 ambapo aliahidi kukabidhi hati kwa waliokwisha kamilisha mchakato huo mwezi ujao.

Katibu wa Kamati ya Urasimishaji Makazi Kivule, Gisiri Magarya alisema mwitikio wa wananchi katika kupima makazi yao ni mkubwa licha ya kuwapo kwa changamoto kadhaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles