31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

WAKIMBIZI WAPEWA MLO MMOJA KWA SIKU

Na MWANDISHI WETU KIGOMA

WAKIMBIZI wa Burundi walioko katika Kambi ya Nduta iliyopo Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wamepunguziwa chakula na kusababisha wengine kuanza kujihusisha na wizi.

Hali hiyo ilibainika hivi karibuni baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kutembelea kambi hiyo.

Mkuu wa Makazi ya Nduta, Peter Bulugu, alisema kupunguzwa kwa chakula kumechangia kuongezeka vitendo vya wizi ndani na nje ya kambi kama vile wizi wa mifugo na mazao mashambani, utekaji, ubakaji na wizi wa taa za mitaani, kambini ambapo 48 kati ya 217 zimeibwa.

Alisema kwa sasa wakimbizi wanaomba hifadhi ni 127,715 kati ya hao 8,743 wameomba kurudishwa makwao.

“Hali ya usalama kambini si nzuri sana kutokana na kuwepo kwa vitendo vya vurugu za mara kwa mara kutoka kundi la wakimbizi linalotaka kurejea makwao.

“Kuna tatizo la chakula kwa wakimbizi, hili linachangia kuwepo kwa wizi ndani na nje ya kambi, kuna malalamiko kutoka vijijini wakimbizi wanakwenda wanaiba mifugo na mazao,” alisema Bulugu.

Mmoja wa wakimbizi ambaye alikutwa akijiandikisha kurudi kwao alisema sababu iliyomfanya achukue uamuzi huo ni kupunguzwa kwa chakula walichokuwa wanapata mwanzoni mpaka sasa kufikia kula mlo mmoja kwa siku.

“Tunapata chakula kidogo yaani kama kimbo mbili tu kwa mwezi mzima, tunateseka sana, tunakula usiku tu hata sasa hivi uji sijanywa. Watoto wetu wanaugua kwa sababu wanashinda njaa,” alisema mkimbizi huyo.

Akiwa kambini hapo, Mwigulu alipata taarifa kuwa wakimbizi 8,743 kutoka katika kambi hiyo wamejisajili kwa hiari yao kurudi Burundi lakini wanakwamishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR).

Kutokana na hali hiyo, alitoa siku saba kwa UNHCR  kukamilisha taratibu za kuwarudisha Warundi walioomba kwa hiari yao kurudi nchini kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles